TANGAZO LA KUITWA KAZINI 25/09/2025
PLACEMENTSeptember 30, 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji
kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 03-11-2024 na tarehe 10-09-2025
kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika
tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye
kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya
nafasi kupatikana
Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, BARUA zao za
kupangiwa vituo vya kazi watazipata kupitia AKAUNTI zao za Ajira Portal kwenye
sehemu ya My Applications, hivyo watapaswa kupakua na kutoa nakala (Download and
Print) barua hizo na Kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa
Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa
na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili
vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo
katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Attachments
Main Attachment
External file link